Sunday, January 20, 2019

Jifunze kutengeneza pesa mtandaoni Make money online

Jifunze kutengeneza pesa mtandaoni Make money online

Making money online is a study like other studies you need to learn many courses to become rich online. Use internet everyday learning new tricks how to make money online.

Jifunze kutengeneza pesa mtandaoni

 Jifunze kutengeneza pesa mtandaoni, make money online, Maisha haya unatakiwa kuwa mbunifu sana. Hali si shwali, siku hizi ukienda sokoni na sh elfu kumi utajikuta umenunua vitu vichache tu na pesa imeisha, Kuna wakati mimi huwa nakuwa na wasiwasi labda pesa yangu huwa inachukuliwa na chuma ulete huko nakoenda kununua bidhaa. Hakika hali ya pesa na matumizi si nzuri.

Kijana hapa ndipo unapotakiwa kutumia akili yako kila siku kubuni vyanzo vya kukuingizia kipato, Vyanzo halali na si vyanzo halamu kama umalaya au kuuza madawa ya kulevya. Kila changamoto ichukulie kama fulsa kwako. Tatizo la mwenzio wewe ligeuze kuwa fulsa ili mradi tu usimwongezee tatizo kwa maksudi ili wewe upate fulsa. Mfano msimba siku zote ni tatizo mwenzio akifiwa bado wewe unaweza kufanya msiba huo kuwa fulsa. Ndiyo msiba unapotokea mtaani kwako wewe unaweza kuchukulia kama fulsa kwa sababu kama ni fundi seremala utauza jeneza, kama wewe unauza sanda siku hiyo utapata pesa, Kama wewe unauza vyakula siku hiyo utauza na bidhaa nyingine au huduma nyingine ambazo lazima kukiwa na msiba zitahitaika. Nadhani sasa umepata concept.

Mitandaoni kuna fulsa nyingi, wenzetu mataifa ya nje walishatajirika sana kwa kutumia mitandao ya kijamii lakini sisi ngozi nyeusi bado sana. Nimefanya utafiti kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii au matumizi ya intaneti kwa jumla na kupata majibu Watu wa ngozi nyeusi hasa maskini ndio wanaongoza kwa kutumia mitandao ya kiamii kwa kupoteza muda. Utaskia vijana wanasema ngoa niingie facebook nipoteze muda kidogo kwasababu nipo bored sana. Sasa ukiingia facebook unatumia pesa, ukiingia instagram na you tube huko ndio hatari unatumia pesa nyingi sana kustream video. Yaani kutazama video za udaku au maisha ya watu waliofanikiwa tayari kama wasanii wa mziki au waigizaji. Siri ipo hapo maskini anatazama video ya diaomond platimum pale you tube maskini anatoa pesa kutazama video wakati Tajiri diamond anaingiza pesa kwa ile video muda maskini anaitazama. Kama ulikuwa hujui ukitazama video you tube unamfanya Yule aliyeitengeneza hiyo video analipwa na Kampuni ya google basi leo nimekujuza.

Ufanye nini ili nawe uanze kulipwa na Kampuni ya google?


Vipo vitu vingi vya kufanya, endelea kusoma makala hii mpaka mwisho ujifunze, Unamiliki simu ya smartphone ya gharama na unajivutia kwa marafiki kuwa una simu kali, Wewe unahisi matumizi ya simu hiyo ndo yameishia hapo kwenye kujisifu kwa marafiki na kupoteza muda kwa kuchat na kukomenti ujinga facebook au instagram. Ukiingia facebook muda huu utaona posts za komedi, utani 90 kati ya mia kumi tu utaweza kuona zinafundisha kitu Fulani au zinatoa taarifa Fulani. Ndugu yangu hiyo simu ni mtaji tosha wa kutengeneza pesa mitandaoni.

Fanya yafuatayo utaingiza pesa na kununua simu kubwa zaidi ya hiyo au kompyuta .

1. Anzisha you tube channel, Kuanzisha you tube channel ni bure ingia www.youtube.com anza kupakia video ambazo unatengeneza. Unaweza dhani kuweka video you tube ni mpaka uwe na studio kama wanazorekodia wasanii wakubwa au uwe na kamera za waandishi wa habari hapana. Simu yako ya smartphone ni studio tosha. Tafuta idea kisha tengeneza video. Unaweza jifunza idea za kurekodi video kwenye milionea Tv channelwww.youtube.com/c/milioneatv Hapo kuna watu wengi watuma video zao ili walipwe kwa idadi ya wanaotazama video zao kwenye channel hiyo. Hakikisha una subscribe kwenye channel hiyo ili ujifunze kurekodi video zinazopendwa na watu.

You tube channel inalipaje?

Hili ni swali la kujua maibu yake kabla hujaanza biashara ya kuendesha Tv ya you tube. Ukishafungua channel yako ya you tube na kuanza kupost video watu watakuwa wanaingia kutazama video zako. Kadili wanavyotazama video zako ndivyo unavyoingiza pesa kutokana na matangazo ya kampuni ya Google huwa yanarushwa kwenye video zako kama umeseti matangazo yaoneshwe kwenye video zako. Kuna vigezo na msharti ya matangazo ya google lakini ni rahisi kuyafuata.

Masharti makubwa ya kuzingatia unapo miliki you tube channel ni haya


1. Usipost video za ngono au video yenye kuonesha picha ya uchi

2. Usibonyeze matangazo ya google kwenye channel yako

3. Usipost video ulizodownload kwenye you tube ambazo si zako.

4. Usiweke mziki wa msanii yoyote kama background au wakati unarekodi video yako chumbani zima mziki mwingine usiingie kwenye video yako kama unataka video hiyo ioneshe matangazo ya Google.

Hayo ni masharti makubwa ambayo unatakiwa kuzingatia ukiwana you tube channel

Google watakutumia pesa toka marekani kwa mfumo wa dola kwa western union ambako utaenda tawi la western union sehemu yoyote mtaani kwako ukiwa na kitambulisho chochote kinachotambulika na serikali ya nchi yako na kuchukua pesa bila tatizo lolote ukifikisha dola 100 sawa na laki mbili na zaidi, Pia unaweza kuchagua nia ya malipo kwa akaunti yako ya benki kama unayo.

Unaweza pia kupata pesa nzuri kwa watu binafsi au makampuni ya nchini mwako ambayo yanataka kutangaza biashara au huduma kwenye online Tv yako. Mfano kampuni ya Vodacom inaweza kutangaza huduma zake kwenye channel yako kwakila video unazoandaa unaweka na video ya tangazo la Vodacom ndani yake.

You tube channe pia inakuwezesha kutangaza live kwa kutumia kompyuta yako au simu. Kama una sherehe kama arusi au kipaimara unaweza teua mtu akutangazie live toka mtaani kwako na watu wataona kila kinachoendelea kwenye channel yako.

Point ya muhimu, Hakikisha unachagua jina zuri la kuipa tv yako na liwe rahisi watu kukumbuka. Usipende kuchangua jina linalotaka kufanana na online tv maarufu ukidhani watu watakuwa nakosea na kuja kwako hapo ni kujidanganya san asana utawafanya wale wanaosearch Tv yako kudondokea kwenye Tv ya mtu mwingine ambayo ni maarufu

2. Anzisha blog. Blog ni nini? Nitatengenezaje blog? Je nitalipia gharama za kuiendesha au ni bure? Blog inaingizaje pesa? Haya yote utajifunza hapa hapa kwenye mtandao huu. Kwa sasa tunaenda mapumziko tutarudi kukuletea elimu hii ya ujasirimali kwa kutumia mitandao. Andika sehemu jina la mtandao huu au blog hii ili usisahau kurudi kujifunza tena.

Kwa sasa anza kulifanyia kazi swala la you tube hapo juu. Hakikisha unapata channel ya you tube haraka iwezekanavyo na kama huui chochote jinsi ya kuitengeneza wasiliana na fundi huyu whatsapp 0652428852 au mtumie sms usipige simu kwakua fundi huyo yupo bize na sms tu nakutengeza you tube za watu, blog na app sasa ukipiga simu unamzimia data na kusitisha zoezi la utengenezaji kwamuda. You tube atakuchaji sh elfu 25 anakuwekea na logo ya Tv bure.

Making money online is a study like other studies you need to learn many courses to become rich online. Use internet everyday learning new tricks how to make money online.


Tuonane kipindi kijacho share hapo chini makala hii iwafikie watu wengi ili waachane na mawazo ya kupoteza muda mitandaoni bonyeza alama ya f au tweet hapo chini. Asante kwa kushare umekuwa sehemu ya watu muhimu wanaopenda Taifa letu liwe na watu matajiri. Pamoja tunaweza pambana na umaskini . Tuonane tena kwenye kipindi kijacho tukiendelea na mada ya Jifunze kutengeneza pesa mtandaoni

0 blogger: