Wednesday, May 14, 2014

WANAOMWIMBIA MUNGU HAWAZEEKI
Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

Umewahi kujiuliza kwa nini waimbaji wengi hawazeeki? Ziko sababu kadhaa za kwa nini hawazeeki na hapa kwa kuwakaribisha nitatoa chache na kuziweka kwenu kwa uchambuzi zaidi.

  1. Kitendo cha kupanua mdomo na kufunga huku ukivuta pumzi na kuimba kunazuia makunyanzi usoni.
  2. Kuimba ni mazoezi.
  3. Kuimba ni kuabudu.
  4. Kuimba kunakuletea nguvu ya Mungu jirani sana.
  5. Kuimba kunafurahisha na kunasambaza hewa ya kutosha mwilini.
Kuimba ni tiba. Na tiba ni muhimu kwa kila jambo linalohusiana na uzima wetu.

JE UKO TAYARI SASA KUIMBA? ANZA SASA